Searching...
Alhamisi, 29 Agosti 2013

KOVA AKIRI WIZI WA KARIAKOO ULIPANGWA,WAIBA MILIONI 792,WAWILI MBARONI

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUMU YA DSM-SULEIMAN KOVA

Muda mfupi baada ya majambazi kuvamia bank ya HABIB AFRICAN BANK kariakoo jijini DSM kamishna wa polisi kanda maalumu ya DSM amezungumza na waandishi wa habari na kukiri kwamba kwa uchunguzi wa awali unaonyesha wizi huo ulipangwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na mazingira ya wizi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari kamishna wa polisi kanda maalumu ya DSM Suleiman Kova amesema wanaoshikiliwa na polisi ni meneja wa benk hiyo tawi la kariakoo pamoja na mlinzi aliyekuwepo zamu muda huo tukio likitokea.
Hata hivyo Kova amesema benk hiyo ilikiuka masharti ya kibenk kuhusiana na ulinzi kwani mlinzi wa benk hiyo hana hata rungu au panga,na meneja anashikiliwa kwasababu alipaswa kubonyeza kitufe cha ulinzi kilichopo humo ndani ofisini kwake ili kuwapa taarifa kampuni ya walinzi lakini kwa makusudi hakufanya hivyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!