B 12
WATANGAZAJI
maarufu Bongo wa Redio Clouds Fm ya jijini Dar es Salaam, Hamis Mandi
‘B 12’, Adam Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’, wamepigwa chini na
kituo hicho, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi
Habari za chini kwa chini kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa uongozi wa Clouds umefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na tabia ya utovu wa nidhamu wa watangazaji hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani yanasema kwamba watangazaji hao wamepigwa chini kwa kosa la kukacha sherehe za maadhimisho ya miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika hivi karibuni katika Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke, Dar.

ADAM MCHOMVU
Risasi
Mchanganyiko lilimvutia waya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu hiyo ambapo
alikiri.
“Ni kweli tumefikia uamuzi wa kuwasimamisha B 12, Diva na Mchomvu baada ya kukiuka baadhi ya makubaliano baina yao na ofisi hivyo kusababisha usumbufu mkubwa ambao ulitulazimu kuingia gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda usiojulikana ingawa watu wengi wamekuwa wakinihoji juu ya hilo lakini watachotakiwa kuelewa ni kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na sheria na taratibu za kuongoza watu wake, sasa hao wamevunja taratibu zetu,” alisema Ruge bila kufafanua zaidi.

DIVA
Alipoulizwa
ni taratibu zipi watangazaji hao walizovunja alisema: “Nashindwa
kueleza kosa la kila mmoja ila naomba nieleweke kuwa hao watangazaji kwa
sasa tumewasimamisha kwa muda usiojulikana wakati tukifikiria cha
kufanya. Muhimu hapo ni kwamba wamekwenda kinyume na tulivyokubaliana.”
KWA HISANI YA GAZETI LA RISASI.
KWA HISANI YA GAZETI LA RISASI.
kidogo naanza kuwafikiria clouds kuwa waweza kuelekea ktk uhalisia wa kuwa chombo cha habari....ile redio inao watangazaji wabovu na watovu kupindukia na wasiojua maadili ya kazi yao!
JibuFuta