Searching...
Jumatano, 25 Oktoba 2017

RAIS WA NIGERIA APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA.


GOODLUCK JONATHAN
RAIS MSTAAFU WA NIGERIA

ABUJA-NIGERIA Rais mstaafu wa Nigera Bw. Goodluck Jonathan, amepewa hati ya kuitwa Mahakamani ili kujibu kesi ya rushwa  inayomkabili msemaji wake wa zamani katika Chama cha Peoples Democratic Party (PDP) Bw. Olisah Metuh.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Shirikisho Bw. Abang Akon anayesikiliza shauri hilo amesema itakuwa ni kama ukiukwaji wa haki za msemaji huyo wa zamani wa Bw. Goodluck kwa usikilizwaji wa haki ikiwa rais mstaafu hatatia saini hati ya kuitwa mahakamani.

Bwana Metuh anakabiliwa na kesi ya kujipatia kiasi cha zaidi ya dola za Kimarekani milioni  moja kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Sambo Dasuki aliyekuwa mshauri wa masuala ya kiusalama Rais mstaafu Jonathan.

Katika utetezi wake mahakamani, msemaji huyo amesema kwamba alipokea fedha hizo kwa maelekezo yaliyotolewa na Jonathan ili kugharamia kampeni za kutetea kiti chake  kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

"Sina namna nyingine yoyote zaidi ya kutia saini hati ya mahakama ya kumlazimisha Rais wa zamani Goodluck Jonathan kufika mahakamani jana Octoba 25, 2017 ili aweze kutoa ushahidi wake" alisema Jaji Abang Okon.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!