Wakati Maelfu ya watu duniani wanajiandaa na sherehe za
kuupokea mwaka mpya wa 2014, huko katika mji wa Sydney nchini Australia
wakiwa tayari wamekwisha upokea mwaka mpya wa 2014 kuliko maeneo mengine
yote duniani na sherehe za kijadi zinaendelea kwa ajili ya sherehe
hizo.
Nchini Japan ambao nao tayari wamekwishaupokea mwaka huu saa mbili nyuma
ya Australia, hivi sasa viongozi dini ya kijadi ya Shinto wamekusanyika
katika mahekalu ya dini hiyo kwa ajili ya sherehe za mwaka mpya.
Hata hivyo katika miji mingine ya nchi za Ulaya sherehe kubwa zitafanyika pia katika miji mbalimbali ikiwemo, Moscow, Paris na London.
Katika nchi za Afrika Mashariki, maandalizi yanaendelea kwa waumini wa
dini mbalimbali kwenda katika nyumba za ibada, kumshukuru Mungu kwa
kuwawezesha kumaliza mwaka 2013 na kuupokea mwaka mpya wa 2014.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.