Searching...
Jumatano, 25 Oktoba 2017

SINGIDA UNITED KURUDI NYUMBANI RASMI.


UWANJA WA NAMFUA SINGIDA
SINGIDA: Timu ya Soka ya Singida United inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kupanda daraja msimu huu, ambayo ilikua inatumia Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma, sasa imelazimika kuhama uwanja huo na kurejea nyumbani kwenye uwanja wao wa Namfua uliopo Mkoani Singida.

Uongozi wa Singida United umesema utaanza kuutumia Uwanja huo wa Namfua mkoani Singida kwa mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Novemba 4, mwaka huu.

Aidha uongozi wa timu ya Singida United wamefikia uamuzi huo ili kupisha marekebisho makubwa yanayoendelea kufanywa kwenye uwanja wa Jamuhuri Mjini Dodoma.
MATENGENEZO YAKIENDELEA UWANJA WA JAMUHURI DODOMA.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba baada ya ukarabati wa kiwango cha juu, uliohusisha pia eneo la kuchezea mpira (pitch), Namfua sasa upo tayari kwa matumizi.

Festo amesema kwamba baada ya Uwanja huo kukamilika, Singida United FC wataanza kutumia Namfua Novemba 4 katika mchezo wao dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga.

Historia ya timu ya Singida United inaanzia kwenye timu nguli kipindi hicho ikijulikana kama Mto Singida FC na inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya pili baada ya kupanda msimu huu, kufuatia awali kucheza ligi hiyo miaka ya 2000.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!