Searching...
Jumatatu, 13 Novemba 2017

BREAKING: HATIMAYE LULU AHUKUMIWA KIFUNGO JELA.

Hatimaye Mahakama Kuu ya Tanzania leo hii tarehe 13-11-2017, imemaliza kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabili muigizaji wa filamu hapa nchini Elizaberth Michael maarufu kwa jina la Lulu, kesi ambayo alikuwa akituhumiwa kumuua aliyekuwa mpenzi wake na muigizaji mwenzake Steven Charles maarufu kama Kanumba.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema muigizaji huyo amehukumiwa kwenda jela miala miwili baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kujiridhisha pasipo na shaka kwamba muigizaji huyo alimuua mpenzi wake huyo bila kukusudia.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Sam Rumanyika, ambapo Jaji huyo amesema kutokana na ushahidi wa kimazingira, mahakama hiyo imethibitisha kwamba Elizaberth Michael ameua bila kukusudia na pia mahakama hiyo imejiridhisha kwamba kutokana na kosa hilo, inafaa muigizaji huyo kutumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Jaji Rumanyika aliwapa nafasi upande wa washitakiwa kujitetea ambapo wakili wa upande huo, Peter Kibatala aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mtuhumiwa kwani yeye ndiye anayetegemewa na familia, lakini ombi lake hilo lilitupiliwa mbali huku akiahidi kukata rufaa kwa madai kwamba hakuridhishwa na hukumu hiyo.

Hata hivyo mara baada ya hukumu hiyo, mama mzazi wa Steven Kanumba alizungumza na waandishi wa habari huku akibubujikwa na machozi huku akimshukuru Mungu na Mahakama hiyo pamoja na serikali ya awamu ya tano kwa kutenda haki katika kesi hiyo na kusema kwamba anaelekea makaburini kuzuru kaburi la mwanae. 


Steven Charles Kanumba alifariki dunia tarehe 07-04-2012 nyumbani kwake Sinza Jijini Dar es Salaam baada ya purukushani chumbani kwake akiwa na mpenzi wake Elizabeth Michale Lulu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kuiweka roho ya Steven Charles Kanumba mahala pema huko peponi. Amen.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!