![]() |
IGP SAID MWEMA |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi. Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mwarakibu Mwandamizi Advera Senso, imesema mabadiliko
hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishina
Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu
ya Polisi Idara ya Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Stephen kutoka Makao Makuu
ya Polisi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Viwanda vya
ndege Kamishina Msaidizi (ACP) Deusdedit Kato amehamishiwa Makao Makuu
ya Polisi na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi
(ACP) Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi. Wengine
ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu
wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa
inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD)."Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi"
0 comments:
Chapisha Maoni