Abiria 28 wakiwemo watoto wanne wamejeruhiwa baada ya basi
walilokuwa wamesafiria la Kampuni ya Shabiby kugongana na Lori tupu la mafuta
na kupinduka katika kijiji cha Kisaki umbali wa kilometa 10 kwenye Barabara Kuu
ya kutoka Mjini Singida kwenda Dodoma.

Taarifa zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi
hilo lenye namba T930BUW aina ya Yutong lililokuwa likiendeshwa
na Dereva wake ambaye
amekimbia mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria
wapatao 48 lilipata ajali hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu
kulipita lori hilo upande wa kulia .
Kawia ufike, alikuwa na haraka ya nini? Serikali inawadhibiti namna gani ma-dreva wa jinsi hiyo? Wanancho pia waanze kutetea maisha yao wanapoona dreva hafanyi yaliyo sawa na kusema kitu hata kama dreva huyo hatasikia. Pole wote waliojeruhiwa na mipango yao yote kubadilika ghafla.
JibuFuta