Searching...
Jumatatu, 23 Oktoba 2017

HUYU NDIYE GAVANA MPYA WA BOT

Prof. Florens D.A.M Luoga-Gavana mteule wa BOT

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akichukua nafasi ya Gavana anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu.

Rais Magufuli ametangaza uteuzi huo, kwenye hafla ya kuwatunuku vyeti vya heshima wajumbe wote wa kamati zote zilizosimamia na kufanya mazungumzo na Barrick Gold Minning.

Leo nimeamua kumteua Gavana katika hawa nilowapa vyeti leo. Nimemteua Prof. Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu mara baada ya Gavana aliyepo kumkabidhi. Prof. Luoga ni Mtaalamu wa Taxation law....alisema Rais Magufuli.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!