TIMU YA TAIFA STARS ILIYOTANGAZWA LEO NA KOCHA SALUM MAYANGA.
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki na Benin Novemba 11,2017 kwenye kalenda ya FIFA, Tanzania itakuwa ugenini kuwakabili Benin.
Kocha Mkuu Salum Mayanga amesema ameita wachezaji 21 watakaoingia kambini Novemba 5 na amejumuisha vijana 3 na jumla yao ni wachezaji 24.
Mayanga ameongeza kuwa ameongeza wachezaji vijana ili kuwajengea uzoefu katika kujenga kikosi
Kikosi kilichotangazwa leo Oktoba 24,2017 na kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga kinaundwa na Makipa ni Aishi Manula(Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).
Mabeki ni Gadiel Michael (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniface Maganga (Mbao FC), Nurdin Chona(Tanzania Prisons), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sonny Sugar, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba), Raphael Daud (Yanga),Simon Msuva (Difaa El Jadidi, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerife, Hispania), Abdul Hilal (Tusker, Kenya), Mohammed Issa (Mtibwa Sugar) na Ibrahim Ajib (Yanga).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Azam), Elias Maguri (Dhofar, Oman) na Yohana Mkomola (Etoile du Sahel, Tunisia).
0 comments:
Chapisha Maoni