Searching...
Jumatano, 29 Januari 2014

TETESI ZA USAJILI LIGI KUU ENGLAND,ARSENAL KULAMBA DUME,ROONEY KUONGEZA MKATABA MAN U,LUKE SHAW KUTUA CHELSEA.

 
JULIAN DRAXLER.
Arsenal wapo mbioni kukamilisha usajili wa kushtukiza wa mchezaji wa Schalke 04 Julian Draxler kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 24.7,usajili ambao unatarajiwa kukamilika kabla ya ijumaa ambapo ndio utakuwa mwisho wa usajili kwa dirisha dogo la January.
 
LUKE SHAW.
Manchester United wamesema wamesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na beki kisiki wa Southampton Luke Shaw ambaye walikuwa wakimuwania kuweka wazi kwamba hana mpango wowote wa kujiunga na Manchester United kwani anajiandaa kujiunga na Chelsea mwishoni mwa msimu huu.
 
TOM INCE.
 Liverpool na Cardiff wameingia vitani kumuwania mshambuliaji wa pembeni wa Blackpool Tom Ince, lakini tayari timu za Stoke na Swansea wamearifiwa kuanza mazungumzo na kinda huyo wa miaka 21.
  GUS POYET
 Kocha wa Sunderland Gus Poyet amemtupia kombora la lawama kocha wa Stoke City Mark Hughes kwa kitendo chake cha kuwalaghai wachezaji wake kiungo Lee Cattermole,25 na mshambuliaji wake Steven Fletcher,26.
 
 NICOLAS OTAMENDI.
 Beki wa Porto Nicolas Otamendi,25,bado anaamini ataihama timu hiyo kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa ijumaa hii hata baada ya mpango wake wa kuhamia Valencia kwa mkopo kukwama,mchezaji huyo anahusishwa kuhamia katika vilabu vya ligi kuu Englanda vya Chelsea,Manchester United na Manchester City.
 
LEWIS HOLTBY.
 Klabu ya Borussia Dortmund wapo katika mazungumzo na klabu ya Tottenham kwaajili ya kumsajili kiungo wao ambaye anaonekana kutokuwa na amani klabuni hapo Lewis Holtby, 23, na kumsajili kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa ijumaa wiki hii.
 
WAYNE ROONEY.
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney, 28, amekubali kuanza mazungumzo na klabu hiyo ili kuingia mkataba mpya utakaomfanya aendelee kukipiga na miamba hiyo ya soka ya England na kumaliza uvumi wa yeye kutaka kutimka kunako klabu hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!