Mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji mwenye asili ya Kenya Devock Orig ameendelea kung'ara katika ulimwengu wa soka baada ya kuifungia timu yake ya taifa goli la kuvutia na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1dhidi ya timu ya taifa ya Iceland.
Hapa Divock Origi (kulia) akishangilia goli lake pamoja na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ubelgiji.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Christian Benteke akimchachafya beki wa Iceland Aron Gunnarsson katika mechi ya kirafiki kati ya timu hizo.
Mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye anatajwa kuwa mlinda mlango bora kwa sasa duniani Thibaut Courtois akijitahidi kuzuia shuti kali langoni lililoelekezwa langoni na Alfred Finnbogason na kumshinda.
Romelu Lukaku akifunga goli kwa urahisi huku mlinda mlango akiwa hayupo langoni.
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku akishangilia ushindi baada ya kuiongoza timu yake kushinda kwa jumla ya magoli 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Iceland.
0 comments:
Chapisha Maoni