IGP ELIZABETH ATUKUNDA AKIZUNGUMZA NA IGP KALE KAYIHURA.
KAMPALA-UGANDA Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, amemteua mtoto Elizabeth Atukunda, mwenye umri wa miaka 11 kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Uganda (IGP) kwa muda wa siku moja.
Elizabeth ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Kampala Parents School amekaimu majukumu ya IGP leo ambapo alikaribishwa ofisini na IGP Kale Kayihura aliyemuachia ofisi.
IGP ELIZABETH ATUKUNDA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA IGP KALE KAYIHURA,MAOFISA WA POLISI,WAFANYAKAZI, ASKARI WATOTO WENZAKE WALIOKUWA WAKIONGOZA MAGARI (TRAFFIC POLICE)
Baada ya kuwasili ofisini katika makao makuu ya jeshi hilo, IGP Elizabeth alipokea ripoti ya utendaji kutoka kwa IGP Kayihura, kisha kukagua gwaride, kabla ya kuelekea barabara ya Jinja kukagua watoto wa kike waliofanya kazi kama Askari barabarani wakiongoza magari.
Pichani ni IGP Elizabeth akipokea ripoti ya utendaji kutoka kwa mtangulizi wake IGP Kayihura. Baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike, uteuzi wa IGP Elizabeth ulitenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na IGP Kayihura.
0 comments:
Chapisha Maoni