Searching...
Jumatano, 18 Oktoba 2017

PIGO KUBWA NCHINI KENYA,KAMISHNA TUME YA UCHAGUZI AJIUZULU AKIWA MAREKANI.

DKT ROSELYN AKOMBE-KAMISHNA WA TUME HURU YA UCHAGUZI KENYA (IEBC)
NAIROBI-KENYA Kamishna wa Tume ya Uchaguzi Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) Dkt. Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu katika tume hiyo ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa urais nchini humo.
Dkt Akombe ametuma taarifa hiyo ya kujiuzulu kutoka mjini New York anakoishi ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya IEBC.
Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.
"Uamuzi wangu wa kuondoka IEBC utawasikitisha baadhi yenu, lakini si kwa sababu nilikosa kujaribu. Nilijaribu kadiri ya uwezo wangu ukizingatia hali na mazingira yaliyopo. Wakati mwingine, unalazimika kusalimu amri na kuondoka, hasa wakati unapoona maisha ya watu yapo  hatarini," amesema kwenye taarifa hiyo.
"Tume sasa imekuwa kama sehemu ya mzozo wa sasa. Tume imo matatani."
"Imekuwa vigumu kuendelea na mikutano ya tume ambapo Makamishna kila wakati wanalazimika kupiga kura kufanya maamuzi kwa kufuata msimamo wao badala ya kuangazia uzito wa jambo linalojadiliwa.
Akombe
"Imekuwa vigumu kutokea kwenye televisheni kutetea misimamo ambayo natofautiana nayo kwa sababu ya kuwajibika kwa pamoja.
"Nimefikia uamuzi kwamba siwezi tena kutoa mchango wa maana kwa Tume na kwa taifa langu kama Kamishna."
Dkt Akombe alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la maafisa waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura.
Dkt Akombe alizuru Nyanza na maeneo ya Magharibi, ambayo ni ngome ya upinzani, wiki iliyopita huku tume hiyo ikijaribu kuwafunza maafisa watakaosimamia uchaguzi huo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!