Searching...
Alhamisi, 12 Oktoba 2017

MLIMA KILIMANJARO WATWAA TUZO YA TATU MFULULIZO.

TUZO YA WORLD TRAVEL AWARDS 2017 KWA MLIMA KILIMANJARO.
Mlima Kilimanjaro umeshinda tuzo ya Kivutio Bora cha Utalii Afrika mwaka 2017. Huu ni ushindi wa tatu mfululizo tangu 2015,katika tuzo hizo zinazoandaliwa na Shirika la World Travel (WTO) ambapo kwa mwaka huu 2017 ni tuzo za 24 tangu kuanzishwa kwake.

MUONEKANO WA MLIMA KILIMANJARO.
Mlima Kilimanjaro ulikua unachuana na vivutio vingine kama Jengo refu la Burj Khalifa (Dubai), Ferrari World (Abu Dhabi), The Great Wall (China), Intramuros (Ufilipino), Las Vergas Strip (Marekani), Machu Picchu (Peru), Spike Island (Ireland) na Mlima Sugarloaf (Brazil)

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!