RAIA WA KOREA KASKAZINI WAKIWA KWENYE FOLENI YA KUINGIA KWENYE DALADALA.
Wakati Taifa la Korea ya Kaskazini linaloongozwa na rais kijana kijana mtukutu Kim Jong Un likijiandaa usiku na mchana kuingia vitani na taifa kubwa duniani la Marekani, taarifa zinasema maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu kila kukicha kama wanavyoonekana hapo pichani wakiwa wamepanga foleni ndefu ya kuingia kwenye daladala.
RAIS KIM JONG UN AKIKAGUA BAADHI YA SIMU ZA MKONONI.
Taarifa zaidi zinasema rais wa nchi hiyo Kim Jong Un analiendesha taifa hilo kibabe kiasi kwamba wananchi hawaruhusiwi kukupata habari zozote nje ya nchi hiyo na hakuna mitandao ya kijamii huku televisheni nyingi zikifungwa na kuachwa moja tu ya serikali huku zingine mbili zikiwashwa siku za mwishoni mwa wiki.
RAIA WA KOREA KASKAZINI AKICHUMA NYASI KWAAJILI YA CHAKULA.
Ukiachilia mbali ubabe huo, lakini taarifa zinasema pamoja na Korea ya Kaskazini kutumia mabilioni ya shilingi kwenye kuimarisha jeshi lake na kutengeneza silaha za nyuklia, bado kuna watu nchini humo wanaishi kwa kula majani kutokana na ugumu wa maisha kama ambavyo mtu huyo anavyoonekana akichuma majani tayari kwa kwenda kupika.
ASKARI WA KOREA YA KASKAZINI WAKISUKUMA GARI
ASKARI AKIFANYA KAZI ZA KIJAMII.
WATOTO WADOGO WAKIFANYA VIBARUA
AMEPUMZIKA
ASKARI AKIJIPUMZISHA KOREA KASKAZINI.
WATOTO WAKICHEZA BARABARANI HUKU MAGARI YAKIENDELEA KUPITA.
0 comments:
Chapisha Maoni