Searching...
Alhamisi, 5 Oktoba 2017

MALAWI KUKIONA CHA MOTO JUMAMOSI.

TIMU YA TAIFA (TAIFA STARS) IKIFANYA MAZOEZI LEO. 

DAR ES SALAAM: Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania,(Taifa Stars) kimeanza mazoezi rasmi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Boko Veterani, eneo la Bunju Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Malawi Jumamosi uwanja wa Uhuru.TFF imesema wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa kwenye timu hiyo wameanza kuwasili tangu jana na watawasili hii leo.Wachezaji hao ni Morel Orgenes (FC Famalicao ya Ureno), Abdi Banda (Baroka FC ya Afrika Kusini), Hamisi Abdallah (Sony Sugar ya Kenya), Abdul Hilal  (Tusker ya Kenya), Simon Msuva (Difaa Hassan El – Jadidah ya Morocco) na Nahodha, Mbwana Samatta (KRC Genk ya Ubelgiji).Kwa ujumla kikosi kiliochoteuliwa na kocha Salum Shaaban Mayanga kwa ajili ya mchezo huo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).Mabeki Gardiel Michael (Yanga), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).Viungo ni Himid Mao ambaye pia ni Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Yanga) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!