Searching...
Jumanne, 26 Septemba 2017

RAILA ODINGA KUDHIBITIWA VILIVYO ENDAPO ATAANDAMANA.


Wakati Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) ukiongozwa na Mgombea wa Urais kupitia muungano huo Raila Odinga ukijiandaa kuandamana hadi kwenye afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) vyombo vya ulinzi na usalama wameweka ulinzi mkali katika jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume hiyo.



Muungano huo wa vyama vya upinzani nchini Kenya wamefikia uamuzi huo wa kuandamana ili kuishinikiza serikali serikali kupitia kwa vyombo vinavyohusika kuwaondoa baadhi ya maofisa wa tume hiyo hasa wakimlenga afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo ya uchaguzi IEBC Ezra Chiloba. 


Aidha Uchaguzi mpya umepangwa kufanyika tarehe 26 Oktoba mwaka huu lakini Nasa wanasema hawatakubali kuingia katika uchaguzi huo kama maofisa hao hawataondolewa ofisini.


Wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini Kenya wanaona kama kitendo cha kufanya mabadiliko katika tume hiyo kitakuwa kigumu kufanyika kutokana na huko siku za nyuma Rais wan nchi hiyo Uhuru Kenyata alisema hakuna mabadiliko yoyote yatakayofanywa katika tume hiyo huru ya uchaguzi.

Muungano huo wa NASA unamtuhumu Afisa Mkuu Mtendaji wa tume hiyo ya uchaguzi IEBC Ezra Chiloba.  kutokana na tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti mwaka huu.

PICHA KWA HISANI YA BBC SWAHILI.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!