MHE. JOB NDUGAI
SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
DAR ES SALAAM: Akizungumza hivi karibuni na East Africa Radio Mh. Ndugai amesema kwamba ingawa huwa kuna adhabu ambazo hutolewa na kamati ya Maadili lakini yeye kama Spika huwa ana adhabu ambazo analazimika kuzitoa kwa kuwa ana mamlaka ndani ya bunge na ndiyo mwenye nafasi ya kutoa au kuzuia ruhusa wakati wa uchangiaji bungeni.
"Zipo adhabu za Kamati ya Maadili ambazo hutolewa lakini pia Spika ndani ya bunge anauwezo na mamlaka ya kutoa nafasi ya kuongea ndiyo maana hata wakati wa kuongea sentensi ya kwanza huwa wanasema Mh. Spika sasa anapotokea mtu ambaye anakudharau na anakutukana hadharani bila sababu kwa nini umpatie nafasi ya kuzungumza mtu huyo? amekuwa shangazi yako? Ni suala la kuheshimiana tu. Kama humuheshimu mtu kwa nini wewe uheshimiwe? Ndugai
Spika Ndugai ameongeza kwamba " Mara nyingi Wabunge ambao huwa wanaofanya vitendo hivyo ni wale ambao wameshaingia bungeni hata mara ya nne lakini utamkuta anamdhalilisha Spika bila sababu na hata akipelekwa kwenye kamati ya maadili akihojiwa na Wabunge wenzake utakuta hana sababu maalumu ya kutoa"
KWA HISANI YA EAST AFRCA RADIO.
0 comments:
Chapisha Maoni