AFRIKA KUSINI:Shirikisho kubwa la vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini (COSATU) wakishirikiana na na washirika wao (SACP) leo wameanza mgomo na maandamano kote nchini yenye lengo la kupinga utawala wa kibaguzi, rushwa pamoja na nchi kutekwa na mafisadi.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na shirikisho hilo, mgomo huo utafanyika nchi nzima lakini zaidi na kwa msisitizo mkubwa utafanyika katika miji mikubwa ya kibiashara ya Johannesburg, Cape Town na Durban.
WAANDAMANAJI WAKIONYESHA BANGO LA KUMTAKA RAIS ZUMA KUONDOKA MADARAKANI.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa COSATU Bw. Bheki Ntshalintshali amesema dhumuni hasa la mgomo na maandamano hayo ni kupeleka ujumbe serikalini na kwa sekta binafsi wa kumshinikiza Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kujiuzulu.
Aidha Bw. Bheki Ntshalintshali ameongeza kuwa shirikisho hilo lina jumla ya wanachama milioni 1.2 na tayari wamewahamasisha wanachama 250,000 ili kuunga mkono harakati hizo.
Naye Katibu Mkuu wa SACP,Bw. Solly Mapaila amesema Rais Jacob Zuma ni kundi la wanyonyaji katika kundi la familia ya Guptas.
0 comments:
Chapisha Maoni