KIKAO CHA KAMATI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)-LUMUMBA, DAR ES SALAAM.
Dar es Salaam: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Taifa ya Chama hicho.
Taarifa iliyotolewa hapo awali na chama hicho inasema mkutano huo pamoja na mambo mengine lakini utakua na jukumu la kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wana CCM ambao wameomba dhamana ya uongozi katika ngazi ya Wilaya.
kwa muhibu wa ratiba ya vikao hivyo ni kwamba Kamati Kuu inakaa tarehe 27-28 Septemba 2017 na Halmashauri Kuu ya Taifa itakaa tarehe 30 Septemba hadi tarehe 1 Octoba 2017.
Vikao hivi vyote vinafanyika katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama hicho Lumumba Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni