BONIFACE JACOB
MEYA WA UBUNGO.
Meya wa Ubungo Mhe. Boniface Jacob amesema leo ameitwa na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma ili kupeleka vielelezo zaidi kuhusu tuhuma alizozipeleka kwenye Sekretarieti hiyo kuhusu sakata la vyeti dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Aidha Mhe Jacob amesema mara baada ya kumaliza mahojiano na Sekretarieti hiyo, atazungumza na vyombo vya habari kuhusu sakata hilo la vyeti pamoja na malalamiko mengine manne.
0 comments:
Chapisha Maoni