Searching...
Jumatano, 27 Septemba 2017

MARUFUKU KUPOKEA WAKIMBIZI KAGERA-UHAMIAJI.


ANNA MAKAKALA.
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI TANZANIA.


KAGERA: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewaagiza viongozi wa Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera kuhakikisha kambi zote za muda zinafungwa mara moja kwani nchi zote za jirani zinazopakana na mkoa huo za Uganda, Rwanda na Burundi zina hali ya amani na utulivu.

Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji hapa nchini Anna Makakala na kusisitiza kwamba mtu yoyote atakayeingia nchini kwa sasa atambulike kama wahamiaji haramu na sio wakimbizi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw. Michael Mntenjele amemuambia Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kuwa kuna watu 223 wanaoomba hifadhi kutoka Burundi na DRC ambao wanapokewa katika kambi ya Rumasi wilayani hapo.

Aidha Kamishna Jenerali Makakala ameahidi kuongeza watumishi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera ili kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaoingia nchini kinyume cha taratibu na sheria.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!