Searching...
Alhamisi, 28 Septemba 2017

NYUMBA ZA POLISI ARUSHA ZATEKETEA.

NYUMBA ZA POLISI ZIKITEKETEA KWA MOTO ARUSHA.

ARUSHA: Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limepatwa na pigo kubwa baada ya zaidi ya nyumba za familia kumi za askari wake kuwaka na kuteketea na moto usiku wa tarehe 27-09-2017 katika eneo la Sekei Mkoani humo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo.

mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alifika eneo la tukio muda mfupi baada ya kutokea kwa moto huo huku Jeshi la zima moto wakifanikiwa kuuzima moto huo ambao hata hivyo bado chanzo chake hakijajulikana.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!