Searching...
Jumatano, 27 Septemba 2017

DUBAI KUANZISHA NDEGE TAX ISIYO NA RUBANI.

NDEGE TAX IKIWA TAYARI KURUKA.
DUBAI; Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isiyo na rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi sehemu za mijini nchini humo.
Ndege hiyo isiyo na rubani yenye nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika Pwani ya Ghuba huku ikitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed. Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani yaVolocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
                                           NDEGE TAX IKIWA ANGANI.
''Utumizi wake utahusisha simu aina ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo unalotaka kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter.
Noel Sharkey ambaye ni mwanasayansi wa komyuta na ambaye pia ni mtaalam wa roboti katika chuo kikuu cha Sheffield alisema kuwa: Changamoo kuu itakuwa vikwazo visivyoepukika kama vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.
KWA HISANI YA BBC.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!