KILIO ARGENTINA,DI MARIA KUKOSA NUSU FAINALI DHIDI YA UHOLANZI
Home
»
Unlabelled
» KILIO ARGENTINA,DI MARIA KUKOSA NUSU FAINALI DHIDI YA UHOLANZI
Michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Brazili imekubwa na jinamizi la majeruhi kwa mastaa wa soka baada ya kipenzi cha soka cha wabrazili Neymar Dosantos kuvunjika sehemu ya mfupa wake wa uti wa mgongo na kuhitimisha ndoto yake ya kuendelea na michuano hiyo.
sasa ni zamu ya miamba ya Soka Argentina itamkosa mchezaji wake nguli
Angel Di Maria katika mechi yao ya nusu fainali dhidi ya Uholanzi baada
ya kuumia goti katika mechi ya robo fainali dhidi ya Ubelgiji.
Di Maria akiwa hoi uwanjani baada ya kuumia mguu wake na kuitia hofu kambi ya Argentina wakati wakikabiliwa na mechi ngumu sana ya nusu fainali dhidi ya Uholanzi jumatano wiki ijayo.
Di Maria alitoka mwenyewe uwanjani tofauti na Neymar aliyetolewa na machela kitendo ambacho kinatafsiriwa kuwa huenda akacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Uholanzi japo kwa dakika 45.
0 comments:
Chapisha Maoni