Ule usemi usemao ukisema cha nini mwenzio anasema atakipata lini ndio unadhihirika kwa aliyekua beki wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole ambaye aliachiwa huru na klabu hiyo chini ya kocha wake mreno Jose Mourinho, ambapo sasa taarifa zinasema kesho jumatatu atasaini mkataba wa miaka miwili ili kuweza kukipiga na miamba ya soka ya Italia klabu ya Roma baada ya kuitumikia klabu ya Chelsea kwa kipindi kirefu cha miaka tisa.
ASHLEY COLE ALIVYONASWA NA MAPAPARAZI AKIVUTA SIGARA KAMBINI.
Ujio wa Mourinho kwa mara ya pili akitokea Madrid kumeonekana balaa kubwa baada ya kocha huyo kumkataa Cole kwa madai ya kiburi kufuatia kumkataza kuvuta sigara kipindi cha ligi lakini Cole alikaidi na kuendelea na tabia yake hiyo hata akiwa kambini.
0 comments:
Chapisha Maoni