Searching...
Jumapili, 6 Julai 2014

HUYU NDIYE MRITHI WA ASHLEY COLE-MOURINHO

JOSE MOURINHO-KOCHA CHELSEA.
Kocha machachari wa klabu tajiri ya Chelsea Mreno Jose Mourinho ameendelea kuhaha kumsaka beki wa kushoto kuchukua mikoba ya Ashley Cole ambapo sasa ameelekeza nguvu na juhudi zake huko katika klabu ya Sporting Lisbon baada ya kuanza mazungumzo rasmi leo kufuatia kutuma ofa ya kitita cha paundi milioni 15 ili kumnasa beki Marcos Rojo ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya mabeki bora kwa sasa duniani na Mourinho kusema wazi kwamba huyu ndiye mrithi wa Ashley Cole.
Chelsea 'open talks with Sporting over £15m Rojo deal'
MARCOS ROJO.
Beki huyo ambaye bado umri wake unamruhusu kucheza kwa zaidi ya miaka kumi kwa sasa ana umri wa miaka 24 na amekua ni moja ya nguzo kubwa ya timu ya taifa ya Argentina huko nchini Brazili na kutoa mchango mkubwa kuifikisha timu yake ya taifa hatua ya nusu fainali.
Jose Mourinho naamini kwamba haitakua kazi rahisi kumpata beki huyo kutokana na vilabu vya Liverpool na Sevilla kutoa upinzani wa hali ya juu kumnasa beki huyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!