Searching...
Jumamosi, 21 Juni 2014

WENGER AENDELEA KUGONGA MWAMBA USAJILI ULAYA.

ARSENAL WENGER.
Wakati kombe la dunia likiwa linaendelea kule nchini Brazili makocha wa timu mbali mbali barani ulaya wapo katika mawindo makali ya usajili ili kuimarisha vikosi vyao msimu ujao. wakati tayari kocha wa Chelsea Jose Mourinho akiwa tayari amenasa saini za wachezaji nguli wawili mshambuliaji wa Hispania mwenye asilia ya Brazil Diego Costa pamoja na kiungo wa timu ya taifa ya Hispania Cesc Fabregas kocha wa Arsenal Arsenal Wenger ameendelea kudondokea pua baada ya mchezaji chaguo la kwanza katika usajili kwa klabu ya hiyo ya Arsenal anayekipiga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambaye pia ni mshambuliaji wa taifa ya Croatia Mario Mandzukic amechomoa kutua Arsenal na badala yake amesema anataka kurejea kwenye klabu yake ya mwanzo ya Wolfsburg.
 

MARIO MANDZUKIC
Mcroatia huyo ambaye tayari ameifungia timu yake ya taifa magoli mawili katika michuano ya kombe la FIFA la dunia inayoendelea nchini Brazili amekua akiwindwa na timu mbalimbali za London kwa miaka mingi amechomoa ofa zote na kuweka wazi kwamba anataka kusalia nchini Ujerumani ili kuendeleza makali yake katika ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Bundesliga.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 aliweka wazi mwishoni mwa msimu uliopita kwamba anataka kuondoka klabuni hapo baada ya kukalia benji kwa muda mrefu na kuonekana kwamba sio chaguo la kwanza la kocha wa Munich.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!