Release No. 112
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 21, 2014
RUKSA UCHAGUZI KUENDELEA SIMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya
kupokea na kuzingatia maombi ya Simba (barua imeambatanishwa), na kwa
kuzingatia Ibara ya 26 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013 limeiruhusu
klabu hiyo kuendelea na mchakato wa uchaguzi wao uliopangwa kufanyika Juni 29
mwaka huu.
TFF inawahimiza wanachama wa klabu ya Simba kuwa
watulivu na wafanye uchaguzi wao kwa amani.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.