Leo ikiwa ni siku ambayo waafrika wengi wanaelekeza macho na masikio yao huko nchini Brazili kuzishuhudia timu mbili za mataifa ya Africa yaani Ghana itakayocheza na Ujerumani saa nne usiku wakati Nigeria wao wataingia uwanjani kumenyana na Bosnia-Herzegovina majira ya saa saba usiku.
Nigeria imekutana na Ujerumani mara mbili na mechi zote Ujerumani walishinda ambapo katika hizo mechi mbili wajerumani waliwafunga Ghana magoli saba na Ghana wamewafunga goli moja tu wajerumani.
Mchezo huo wa kundi G utachezwa katika uwanja wa Stadio Castelao uliopo katika mji wa Fortaleza,uwanja huo umejengwa mwaka 1973 na una uwezo wa kuchukua watazamaji 60342.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Sandro Ricci kutoka brazili,ambapo atasaidiana na mshika kibendera Emerson De Carvalho na Marcelo Van Gasse wote kutoka nchini Brazili na mwamuzi wa mezani atakua ni Victor Carrillo kutoka nchini Peru.
huu ndio msimamo wa kundi linaloaminika kuwa ndilo kundi la kifo katika kombe la dunia 2014
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.