
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani Kagera imewavua udiwani madiwani sita 6
kati ya nane 8 wa manispaa ya Bukoba baada ya kupoteza sifa ya kuwa na
nyadhifa hizo kutokana na utoro wa kutohudhuria vikao vya madiwani.
Mgogoro
huo ulisababisha fedha za miradi ya maendeleo kurejeshwa serikali kuu
bila kutumika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
Aidha
madiwani hao hawataruhusiwa kugombea tena. Miongoni mwa madiwani hao 5
ni kutoka chama chama cha Mapinduzi na mmoja kutoka CUF
Ikumbukwe
kuwa palikuwepo na mgogoro kati ya mbunge wa jimbo la Bukoba Balozi
Khamis Kagasheki na aliyekuwa mayor wa manispaa hiyo Dr. Anathory Amani
jambo lililosababisha madiwani wafuasi wa Kagasheki kususia vikao vya
madiwani.
Na Hilali Ruhundwa- Malunde1 blog-Kagera
0 comments:
Chapisha Maoni