Searching...
Ijumaa, 20 Juni 2014

ARSENAL KUIBOMOA CHELSEA,YAJIPANGA KUMSAJILI NYOTA WA MOURINHO.

 
Branislav Ivanovic
Katika hali ya kushangaza na kustua,timu ya Arsenal maarufu kama The Gunners wamejiaminisha kwamba wanaweza wakaibomoa Chelsea kwa kumsajili beki wao kisiki raia wa Serbian Branislav Ivanovic kwa kitita cha paundi milioni7.
Arsenal wamefikia uamuzi huo kutokana na kuamua kumuuza nahodha wao Thomas Vermaelen, ambaye anajiandaa kujiunga na mashetani wekundu Manchester United. Inaaminika kwamba kocha wa Arsenal Arsene Wenger ni shabiki mkubwa na kipenzi cha Mserbian huyo ambaye anaweza akacheza nafasi mbili kati ya beki wa kati au beki wa kulia.
Ikumbukwe kwamba Arsenal tayari wamempoteza beki wao mwingine Bacary Sagna ambaye amejiunga na mabingwa wa ligi kuu England Manchester City kwa mkataba wa miaka mitatu.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!