Zaidi ya kilo 200 za madawa ya kulevywa aina ya heroin yamekamatwa
na kikosi cha polisi wanamaji katika bahari ya hindi yakisafirishwa
kutokea nchini irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya
Irani na Pakistani.
blog hii imefika katika eneo la bandari ya Dar es Salaam
na kushuhudia jahazi hilo linalosadikiwa kutokea nchi ya Irani likiwa
na shehena hiyo ya madawa ya kulevya ambapo kamanda wa polisi kikosi cha
wanamaji Mboje Kanga akielezea.
Tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya
saa sita usiku waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili
wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala kingereza na jahazi lao
halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevywa
godfrey nzowa amesema jahazi Hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosa cha
polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na
mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua
walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya Aliyoyataja kuwa ni aina ya
Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
Matukio ya kukamatwa kwa dawa za kulevywa nchini
yamekuwa endelevu na kipindi hiki mbinu imebadilika tofauti na awali
amabapo mengi yamekuwa yakikamatwa kwenye bandari kavu ambapo mwaka juzi
zaisi ya kilo 200 zilikamtwa bandari kavu ya Lindi lilo 179 bandari
hiyo hiyo,kilo 97 na kilo 81 zilikamtwa kwenye bahari ya hindi yakitokea
Irani.
0 comments:
Chapisha Maoni