Searching...
Alhamisi, 16 Januari 2014

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA 23 WAJERUHIWA VIBAYA KWENYE AJALI MBEYA

Hivi ndivyo ilivyokuwa ajali hiyo iliyohusisha Lori na Coaster katika eneo la Mbalizi

Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 10:45 leo jioni katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea Mbalizi
Baadhi ya askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo katika Lori, hata hivyo askari hao walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa hizo.
Mmoja wa majeruhi wa ajali akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa matibabu.
Wauguzi wa huduma ya haraka katika hospitali ya Rufaa Mbeya wakimpatia huduma mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo
WIMBI la ajali katika miezi ya Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya ajali nyingine kutokea mkoani Mbeya leo jioni majira ya saa 10:45 katika  mtelemko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 23.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya Coaster na Lori la mizigo yalikuwa yakielekea njia ya Tunduma kutokea Jijini Mbeya ambapo lori hilo linadaiwa kuharibika mfumo wa breki likiwa mtelemkoni.
Lori hilo la mizigo aina ya SCANIA lenye namba za usajili T 101 CRL na trela lenye namba za usajili T 859 BZW ambalo lilibeba bidhaa mbalimbali za madukani liliigonga Coaster yenye namba za usajili T 910 BFB na kusababisha magari hayo kupinduka.

0 comments:

Chapisha Maoni

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!