MIRKO VUCINIC.
Arsenal wamekubaliana na klabu ya Juventus kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wao mkongwe Mirko
Vucinic,mchezaji huyo wa kimataifa wa Montenegro anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo alhamisi ili kuanza kibarua chake kunako Emirates.
PEP GUARDIOLA
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amefungua milango kwaajili ya mazungumzo ya kinda wake Toni
Kroos kujiunga na Manchester United. amesema kiungo huyo mjerumani mwenye umri wa miaka 24 anaweza akajiunga na Manchester United muda wowote kama wataafikiana kwasababu katika soka leo unakua hapa kesho pale na maisha yanaendelea.
KURT ZOUMA.
Timu ya St Etienne wanaendelea na mazungumzo na klabu ya Chelsea kwaajili beki wao wa kati Kurt Zouma ambapo matajiri hao wa London wametuma ofa nono ya paundi milioni 18 kwaajili ya kuinasa saini ya kinda huyo wa kimataifa wa ufaransa.
ISAAC CUENCA.
Timu za Liverpool na Arsenal wameingia vitani kwa mara nyingine kuwania saini ya mshambuliaji wa Barcelona Isaac Cuenca.
0 comments:
Chapisha Maoni