Searching...
Alhamisi, 30 Januari 2014

JUSTINE BIEBER AFUNGULIWA MASHITAKA

Mwanamziki mashuhuri wa muziki wa 'pop' kutoka Canada Justin Bieber amefunguliwa mashtaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari la kukodisha mwezi Disemba mwaka uliopita.
Bwana Bieber aliye na umri wa miaka 19 alikaribishwa katika kituo cha polisi cha Toronto na kikosi kikubwa cha wapiga picha za televisheni pamoja na unyende wa mashabiki wake chipukizi.
Amefunguliwa mashtaka chini ya juma moja baada ya kukamatwa mjini Florida marekani kwa shutuma za kuendesha gari akiwa mlevi na mashtaka mengine.
 
Mwanasheria wa Marekani anayemwakilisha mwimbaji huyo amesema mteja wake hana makosa.
Kwa mujibu wa polisi wa Toronto, yapata saa 02:50 saa za Canada tarehe 30 Disemba, gari la kifahari liliwasili kumchukuwa bwana Bieber na wenzake watano katika kilabu moja ya starehe ili kuwarejesha katika chumba chao cha hoteli.
Na wakati walipokuwa njiani, dereva huyo pamoja na mmoja wa abiria wake, aliyetajwa kama bwana Bieber, wanasemekana kuanza kufokeana maneno makali.
Abiria huyo "alimgonga dereva wa limousine hiyo kwenye kisogo mara kadhaa", polisi wamesema.
Dereva huyo anasemekana kusimamisha gari lake na kisha kutoka nje na kuwaita polisi. Mshukiwa 'alichana mbuga' kabla ya polisi kuwasili.
Bwana Bieber alijisalimisha kwa polisi Jumatano. Anatarajiwa kufikishwa kizimbani tarehe kumi mwezi Machi mwaka huu.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!