JERMAIN DEFOE.
Mshambuliaji wa timu ya Tottenham Jermain Defoe, 31, yupo mbioni kujiunga na klabu ya Toronto FC inayoshiriki ligi kuu ya soka ya marekani maarufu kama Major League kwa kitita cha paundi milioni 6.
CLAUDIO MARCHISIO
Manchester United wapo tayari kuingia katika vita ya kumwania kiungo mchezeshaji wa Juventus Claudio
Marchisio, 27, kwa kitita cha paundi milioni 20 japokuwa kiungo huyo ameweka wazi kwamba anataka kubakia Turin.
CHEIKHOU KOUYATE.
Vilabu vya Arsenal na Liverpool wapo katika vita vikali vya kuiwania saini ya beki kisiki wa Anderlecht Cheikhou
Kouyate, 24, ambapo wakala wake amesema wapo kwenye mazungumzo na vilabu vyote viwili hivyo vya England.
ALVARO MORATA
Arsenal italazimika kulipa ada ya uhamisho wa mkopo wa paundi milioni 1.7 ili kuweza kuipata huduma ya kinda wa Real Madrid mshambuliaji
Alvaro Morata, 21.

TOM INCE
Timu ya Swansea City wanaamini wataweza kuwapiku Cardiff na Crystal
Palace katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji nguli wa Blackpool Tom Ince, 21, ambaye yupo sokoni kwa kitita cha paundi milioni 4.
ERIK LAMELA.
Juventus wanapanga kuingia Tottenham kwaajili ya mazungumzo ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa pembeni Erik Lamela, 21,mwishoni mwa msimu huu
0 comments:
Chapisha Maoni