Alvaro Negredo kushoto akifurahia goli lake la kwanza kati ya magoli matatu aliyoyafunga yeye mwenyewe na kuhitimisha mechi hiyo ya nusu fainali ya Capital One kufikia 6-0 dhidi ya vibonde vinavyochechemea kunako ligi kuu England West Ham United.
Mchezaji wa kimataifa wa Ivory Cost Yaya Toure akipigilia msumari wa tatu katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya West Ham katika mechi ya nusu fainali ya kombe la Capital One.
Kocha wa West Ham Sam Allardyce (Big Sam) akiwa haamini macho yake baada ya wachezaji wake kukubali kipigo cha kudhalilisha cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City.
0 comments:
Chapisha Maoni