MARAIS WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI-KUTOKA
KUSHOTO: UHURU KENYATTA, YOWERI MUSEVENI NA PAUL KAGAME.
Mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani kutoka nchi za Uganda,Rwanda na
Kenya wametia saini makubaliano kuweka himaya moja ya ulinzi miongoni
mwa nchi hizo.
Hii ni mara ya kwanza kuwepo kwa mkataba huo na hii ina maana nchi moja
ikipata matatizo ya usalama nchi nyingine zitakuwa na uhuru wa kuingilia
kati na kusaidia. Kikao cha mawaziri hao kilitanguliwa na kile cha
wakuu wa majeshi na polisi kutoka nchi hizo ambacho pia kilitathmini
changamoto za kiusalama kwenye eneo hilo na jinsi ya kuimarisha
ushirikiano miongoni mwa mataifa hayo. Kutoka Kigali mwandishi wetu
Sylivanus Karemera anaripoti zaidi. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama
ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:
Sylivanus Karemera-BBC
0 comments:
Chapisha Maoni