DIEGO COSTA AKIWA KAZINI.
Taarifa za uhakika kutoka nchini Hispania zinasema kwamba klabu ya Atletico Madrid imekubaliana na klabu ya Chelsea kumuachia mshambuliaji wao nguli Diego Costa kutua darajani mwishoni mwa msimu huu.
Gazeti la Hispania la ‘La Sexta’ limemnukuu msemaji wa Diego Costa Francois Gallardo – ambaye amesema Chelsea tayari wamekubaliana na Atletico Madrid kumnunua mshambuliaji huyio kwa kitita cha paundi milioni 32, ambapo pia aliongeza kwamba imekua rahisi kwa Chelsea kumnasa mshabuliaji huyo baada ya Atletico kugundua kwamba hawawezi kumshawishi mchezaji huyo kusalia kunako klabu hiyo
0 comments:
Chapisha Maoni