Kiungo wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Chelsea Juan Mata leo hii anatarajiwa kufanyiwa vipimo kunako Manchester United baada ya Chelsea kukubali kumuuza kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 37.
Manchester United wanaonekana kulamba dume mara tu baada ya kocha wa Chelsea Jose Mourinho kumuambia Mata kwamba atafute timu kwasababu hana mpango wa kumtumia katika klabu yake ya Stamford Bridge.
David Moyes amekubali kumuongezea Mata mshahara mara mbili ya ule anaoupata pale Chelsea kutoka paundi 70,000 hadi paundi 140,000 na tayari baba yake na Mata yupo England kukamilisha usajili huo.
0 comments:
Chapisha Maoni