Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi,baada ya Manchester United kufungwa 2-1 na Sunderland ugenini wiki iliyopita,usiku wa leo imefungwa kwa penalti baada ya kwenda dakika 120 kwa uwiano wa magoli 3-3 na kisha kupoteza kwa penalti 1-2
ambapo wachezaji wa Man U walionekana kupotezana hadi wakati wa penalti ambapo walipata moja tu kati ya 5 huku 2 wakipaisha juu ya lango na mbili zikiishia mikononi mwa golikipa wa Sunderland.
kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alionekana kukerwa sana na matokeo hayo ambapo baada ya filimbi ya mwisho alionekana kuinamisha kichwa chini akiwa haamini macho yake.
Wachezaji wa Sunderland wakishangilia baada ya golikipa wao kuipangua penalti ya mwisho ya Man U na kuwatupa nje na kuzima ndoto za Moyes za kutwaa taji la Capital One.
(mechi hii imechezewa uwanja wa nyumbani wa Man U-Oldtraford na kuendeleza rekodi mbaya ya kufungwa nyumbani)

0 comments:
Chapisha Maoni