Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya KCC ya Uganda, Kawooya Fahad,
Kombe la Mapinduzi baada kumalizika kwa mchezo wa Fainali wa Kombe la
Mapinduzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo jioni.
Katika mchezo huo KCC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa
katika dakika ya 7 ya mchezo.
Meza kuu ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar.. na baadhi ya viongozi.
Kipa wa Simba Ivo Mapunda, akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Manahodha wa timu hizo, Amri Kiemba na Kawooya Fahad, wakichuana kuwania mpira.
Ramadhan Singano wa Simba akichuana na Magoola Omar.
Sehemu ya mashabiki na viongozi wa waliohudhuria mtanange huo.
Sehemu ya mashabiki wa Simba waliohudhuria mtanange huo.
Mwenyekiti
wa Simba 'Anayeshinikizwa kuachia madaraka' Aden Ismail Rage, (wa tatu
kuli mbele) akiwa ni mmoja kati ya waliohudhuria mtanange huo.
Kocha wa Simba, Lugalusic, akitoa maelekezo kwa beki wake Joseph Owino.
Kocha akiendelea kutoa maelekezo......
Mshambuliaji wa Simba Amis Tambwe, akijikunja kupiga mpira wa kichwa.
Mabeki wa Simba Issa Rashid (kulia) na Joseph Owino, wakimdibiti mshambuliaji wa KCC, Odur Tony.
Kocha wa Simba, Logalusic akiwapa Big Up wachezaji wa KCC baada ya mchezo huo kumalizika.
Baada
ya bao hilo dakika mbili baadaye Kocha wa Simba, Logalusic, alianza
kufanya mabadiliko kwa kumtoa beki Haruna Shamte na kumuingiza William
Lucian, na dakika ya 29, alimtoa Awadh Juma na kumuingiza Ramadhan
Chombo, na kumtoa Haruna Chanongo na kumuingiza Betram Mwombeki na
baadaye tena alimtoa beki, Issa Rashid na kumuingiza Uhuru Seleman.
Pamoja na mabadiliko hayo bado hayakuweza kuzaa matunda na kubadilisha
matokeo hivyo hadi mwisho wa mchwzo KCC 1 Simba 0.
KWA HISANI YA SUFIAN MAFOTO.COM
KWA HISANI YA SUFIAN MAFOTO.COM
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.