Searching...
Jumatatu, 13 Januari 2014

JUAN MATA HAUZWI - MOURINHO


Mata still key for Chelsea, says Jose
JUAN MATA.
Pamoja na taarifa nyingi kuzagaa kwamba mchezaji bora wa chelsea mara mbili Juan Mata anaondoka klabuni hapo,leo hii kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho ameibuka na kuzima uvumi huo kwa kusema kwamba mchezaji huyo ni muhimu sana kwenye timu hiyo tofauti na watu wanavyofikiria.
Mata anaonekana kukata tamaa ya kupata namba klabuni hapo baada ya wahezaji wenzake Eden Hazard, Oscar na Willian kuonekana kuwa chaguo la kwanza la Mourinho
Mata still key for Chelsea, says Jose
MATA NA SCHURRLE.
‘Tunahitaji wachezaji,kama uliona mechi kati ya Hull ilikuwa ngumu sana,tulikua 0-0 lakini Mata alivyoingia,alibadilisha kabisa mchezo na tukafunga na kuibuka washindi,hapo ndipo akili yangu ilikuja kubadilika kabisa kuhusu Mata.
‘kusema ukweli tunawahitaji sana Mata na  Andre Schurrle, tunawahitaji hawa wachezaji,na hatuwezi kuwauza" alisema Mourinho.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!