Searching...
Jumapili, 12 Januari 2014

EDEN HAZARD ANA THAMANI YA ZAIDI YA PAUNDI MILIONI 100-MOURINHO.

 
EDEN HAZARD.
Kocha mkuu wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amepasua jipu kwa kummwagia sifa tele kiungo wake mbelgiji Eden Hazard kwamba ni mmoja kati ya wachezaji ghali duniani na kufananisha thamani yake kuwa ni zaidi ya paundi milioni 100.
 
 JOSE MOURINHO AKIMPA HAZARD MAELEKEZO.
Mourinho amesema katika ulimwengu wa soka wa sasa,ili uwe mvchezaji bora duniani unapaswa kufanya mazoezi kwa bidii na kwa nguvu,kuwa na nidhamu ndani na nje ya uwanja na kusikiliza yale mwalimu anayokuagiza ufanye unapokuwa uwanjani,vigezo ambavyo Mourinho amesema kiungo wake Hazard anavyo vyote.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!