Sharon alizaliwa katika eneo la Palestina mwaka 1928 . Alipigana katika
vita kati ya waarabu na wapalestina kati ya mwaka 1948-49 na kuongoza
majeshi ya Israel mapema miaka ya hamsini.
Aliyekuwa kiongozi wa Israel Ariel Sharon, aliyefariki dunia tarehe 11.01.2013 akiwa na umri wa
miaka 85. Alipatwa na Kiharusi Januari mwaka 2006 na tangu hapo akawa
anatumia mashine kupumua. Hatimaye viungo vya mwili wa Sharon vimekuwa
vikiathirika kutokana na hali yake mahututi.
Mwaka 1971, Sharon aliamuru kuharibiwa kwa nyumba 2,000 za wapalestina
katika juhudi zake za kukabiliana na wapiganaji wa kipalestina waliokuwa
wanapigania uhuru wa Palestin.
Mwaka 1973, Sharon alihudumu katika jeshi wakati wa vita vya Mashariki
ya Kati. Kama waziri wa kilimo chini ya utawala wa Menachem Begin,
aliunga mkono sera ya kujenga makazi ya walowezi katika eneo la
Palestina.
Kama waziri wa ulinzi Sharon alioongoza uvamizi dhidi ya Lebanon mwaka
1982. Alifanya hivyo ili kuwezesha wanajeshi wakristo wa Phalangist
kuingia katika kambi za Sabra na Shatila kuwasaka wapiganaji wa PLA.
Maelfu ya watu walifariki katika vita hivyo, na kupelekea wapalestina
kumuita Sharon muuaji. Waisraeli, 400,000 waliandamana kupinga matamshi
hayo
Sharon aliungwa mkono na mkewe wa pili Lili na wanawe Omri na Gilad.
Mkewe wa kwanza Margalit alifariki katika ajali ya barabarani, mwaka
1962. Mwanawe Margalit alifariki mwaka 1967 katika tukio la
ufyatulianaji risasi. Naye Lili alifariki mwaka 2000
Sharon alijiondoa katika siasa na wala hakuonekana sana hadharani akitoa
matamshi ya kisiasa baada ya kustaafu. Lakini mapema miaka ya 1990,
nyota yake ilianza tena kung'aa na mwaka 1999 alichaguliwa kama kiongozi
wa chama cha Likud.
Sharon alianza kuwaondoa walowezi kutoka katika ukanda wa Gaza na maeneo
machache ya Ukingo wa magharibi mwaka 2005. Kitendo chake hicho
kiliwaghadhabisha baadhi ya wafuasi wake na kumlazimisha kudhibiti
usalama zaidi
Mnamo mwezi Septemba mwaka 2000, huku hali ya taharuki ikishuhudiwa,
ziara ya Sharon katika Hekallu la Mount/Dome eneo takatifu kwa wakristo
na waisilamu, ilizua utata na kuchochea harakati za waplestina dhidi ya
Israel.
Mwaka 2001, Sharon alishinda uchaguzi mkuu baada ya kuwaahidi waisraeli
kuwa angekabiliana vilivyo na mashambulizi yoyote kutoka kwa waplestina.
Lakini uhasama ulikithiri na Sharon akachoka kuwa mvumilivu kwa
wapalestina
REST IN PEACE SHARON.
0 comments:
Chapisha Maoni