
MAREHEMU HASSAN AL-RDOUI-ALIYEKUWA NAIBU WAZIRI WA VIWANDA WA LIBYA.
Naibu Waziri wa viwanda nchini Libya ameuawa kwa
kupigwa risasi wakati alipokuwa ziarani mjini Sirte Mashariki mwa
Tripoli ambako alizaliwa.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu
wasiojulikana walimfyatulia risasi kadhaa Hassan al-Droui karibu na
soko rasmi mjini humo.
Ni mauaji ya kwanza ya afisaa wa serikali ya mpito ya Libya.
Libya imekuwa ikikumbwa na vurugu tangu kuondolewa mamlakani kwa hayati Muammar Gaddafi mwezi Oktoba mwaka 2011.
Sirte ilikuwa ngome ya mwisho ambako mapigano
yalitokea wakati wa harakati za mapinduzi ya Muamar Gaddafi ambaye
alikamatwa na kupigwa risasi akijaribu kujificha kutoka kwa waasi.
Bwana al-Droui alikuwa mwanachama wa zamani wa baraza la mpito lililosimamia kipindi cha mpito baada ya Gadaffi kuuawa.
Aliteuliwa kama naibu waziri na waziri mkuu wa
kwanza wa mpito na kuendelea kushikilia wadhifa huo hata baada ya Ali
Zeidan kuchukua mamlaka.
CHANZO NA BBC
0 comments:
Chapisha Maoni