Searching...
Jumapili, 12 Januari 2014

TETESI ZA UHAMISHO WA DIRISHA DOGO ULAYA,MAN U,CHELSEA,MAN CITY,REAL MADRID,ARSENAL ZIPO HAPA

 
 NEMANJA MATIC.
Chelsea wanajiandaa kutoa kitita cha paundi milioni 21 kumsajili kiungo wa timu ya Benfica ya Ureno Nemanja Matic, 26, katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo la januari,Matic alijiunga na klabu hiyo ya Ureno januari 2011 akitokea Chelsea,sasa ni kama anarejea nyumbani.
 
LUKE SHAW.
Manchester City Wapo tayari kulipa kitita cha paundi milioni 30 kumsainisha mlinzi kisiki wa Southampton Luke Shaw, 18,kitita ambacho kitakua ni rekodi ya dunia kwa mchezaji wa nafasi ya beki,rekodi iliyopo hadi sasa kwa mlinzi kununuliwa na kitita kikubwa ni kile aliyenunuliwa Dani Alves cha paundi milioni 29.5 mwaka 2008 kutoka Sevilla kwenda Barcelona.
 
JOLEON LESCOTT.
Timu ya West Ham wamekubaliana na timu ya Manchester City kumsajili beki wa kati Joleon Lescott lakini makubaliano hayo huenda yasifanikiwe baada ya matajiri hao wa jiji la Manchester kustuka na kudai kwamba makubaliano hayo yatajulikana rasmi januari 20 baada ya kuona upepo wa usajili wa dirisha dogo utakavyowaendea.
 Better call Saul: In-demand Niguez is on loan at Rayo Vallacano from Atletico Madrid
SAUL NIGUEL.
Arsenal na Chelsea wapo vitani kuwania saini ya kiungo wa kati wa klabu ya Atletico Madrid  Saul Niguel kinda mwenye umri wa miaka 19 lakini mwenye kipaji cha hali ya juu. 
 
FABIO COENTRAO.
 Manchester United wanajipanga kutuma maombi Real Madrid defender ya kumsajili kwa mkopo Fabio Coentrao, 25, mwishoni mwa msimu huu,japo Moyes anaamini itakua ni vigumu sana kwa kocha wa Madrid kukubali ombi hilo.

PAUL POGBA.
Manchester City wanataka kumsajili mchezaji wa zamani wa majirani zao Manchester United Paul Pogba. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anayecheza nafasi ya kiungo kwa sasa anakipiga na miamba ya soka ya Italia kibibi kizee cha Turin Juventus.
 
ETIENNE CAPOUE.
Kocha mkuu wa Tottenham Tim Sherwood amesema hana furaha kutokana na tabia za baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na yupo tayari kumuuza kiungo wake mwenye umri wa miaka 25 Etienne Capoue, 25. 
 
ANDERSON.
Kiungo wa Manchester United Anderson, 25, yupo mbioni kujiunga na klabu ya Fiorentina ya Italia Fiorentina, wakati washambuliaji wa pembeni Luis Nani, 27, na Wilfried Zaha, 21, wanatarajiwa kuuzwa kwa mkopo kwa vilabu vya Sporting Lisbon na Cardiff City mapema mwezi huu.

JULIAN DRAXLER.
Arsenal wamepata nguvu mpya ya kumsajili mshambuliaji wa nguli wa timu ya Schalke 04  Julian Draxler, 20, baada ya kugundua kwamba gharama yake ni paundi milioni 40.
 
PAPISS CISSE.
 Mshambuliaji wa Newcastle United Papiss Cisse, 28, anataka kuihama timu hiyo ili akajiunge na timu ya Qatar japo timu hiyo ya Tyneside i kumuuza vinginevyo walipwe kwanza kitita cha pundi milioni 9 walizomnunulia mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!