Searching...
Jumatatu, 9 Desemba 2013

HALI SIO SHWARI AFRIKA YA KATI,UFARANSA YAINGILIA KATI


 MAJESHI YA UFARANSA YAKIPIGA DORIA JIJINI BANGUI
Hali katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika kati-Bangui,bado inatisha baada ya mapigano ya umwagaji damu kati ya makundi ya imani tofauti za kidini.Hata hivyo jeshi la Ufaransa linasema hali bado inatisha.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema mpango wa kuwapokonya silaha wafuasi wa makundi tofauti ya wanamgambo unaanza hii leo.Ameonya jeshi la Ufaransa linaweza kutumia nguvu kuwalazimisha wanamgambo wazisalimishe silaha zao.Katika mahojiano na kituo cha matangazo cha RTL waziri huyo wa ulinzi wa Ufaransa amesema baadhi ya makundi ya wanamgambo wameanza kuchanganyika na raia wa kawaida na kusababisha "vurugu".
WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI NICOLAS TIANGAYE.
Wakaazi wa mji mkuu Bangui wamezungumzia kuhusu milio ya hapa na pale ya risasi katika baadhi ya mitaa ya mji huo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirika la haki za binaadamu la Jamhuri ya Afrika kati,Joseph Bindoumi,wanamgambo wa Seleka ambao wengi wao ni waislam,bado wangalipo mjini Bangui.
"Hali ni tulivu lakini inatisha" amesema msemaji wa jeshi la Ufaransa kanali Gilles Jaron akiwa mjini Paris.Ufaransa imeamua kutuma jumla ya wanajeshi 1600 katika Jamhuri ya Afrika kati,1200 kati yao mjini Bangui.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!